Utafiti wa mpya uliofanyika Muheza, Tanga Tanzania, umeonyesha kwamba mafuta ya asili yanayotokana na mmea wa Chenopodium ambrosioides yana uwezo mkubwa wa kuua mbu wanaosambaza magonjwa kama malaria, dengue, na matende. Hii ni habari njema hasa kwa wakati huu ambapo mbu wamekuwa na usugu dhidi ya dawa za kuua wadudu.

Kutoka kwenye ripoti ya utafiti huo, mafuta haya yalifanya kazi vizuri zaidi kuliko viambata viliyopo kwenye dawa zinazotumika kwa muda mrefu. Kutokana na matokeo ya awali ya utafiti huu, mafuta ya mmea huo inawezakana yakachangia kuja na suluhisho la haraka la kupunguza idadi ya mbu na kuzuia magonjwa.

Hata hivyo, utafiti pia ulionyesha kwamba baadhi ya mbu wameanza kuwa sugu dhidi ya dawa za kawaida. Hii inaonyesha hitaji la kuboresha mbinu za kudhibiti mbu kwa kutumia njia mbadala kama mafuta ya asili kutoka kwenye mimea.

Utafiti huu umetoa mapendekezo muhimu kwa sasa na baadaye. Moja ya mapendekezo hayo ni kuwa, watafiti wanapaswa kufanya kazi na wadau mbalimbali wa viwanda na afya kutengeneza bidhaa za gharama nafuu kwa matumizi ya nyumbani, kama vile dawa za kupaka au dawa za kufukizia.

Mwisho, ni muhimu kwa serikali na wadau mbalimbali wa afya kuanza kuelimisha jamii kuhusu ufanisi wa dawa za asili. Hii itasaidia kukabiliana na changamoto ya magonjwa ya mbu kwa njia salama na endelevu.

Kwa ufupi, utafiti huu unaweka Tanzania katika ramani ya utafiti wa dawa za asili dhidi ya mbu. Kwa kutumia rasilimali za asili kama Chenopodium ambrosioides, tunaweza kupambana na magonjwa ya mbu kwa njia bora zaidi.

Je, wewe una uzoefu wowote na dawa za asili za kuua mbu? Tushirikishe mawazo yako kwenye comments!